Fomu ya Idhini ya Dataza Bayometriki ya World Foundation
Fomu ya Idhini ya Data za Bayometriki ya Asasi ya World
Muhtasari. Muhtasari huu unakusudiwa kukusaidia kuelewa kwa haraka kile ambacho unaombwa kukubali unapothibitisha kwenye kifaa cha Orb. Ikiwa ungependa maelezo zaidi, tafadhali pitia maelezo kamili ya idhini, yaliyo hapa chini. Si lazima ukubaliane na Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki ili kushiriki katika mradi wa World. Haya ndiyo machaguo yako: (Baadhi ya machaguo hapa chini (na haswa Umiliki Data) huenda hazipatikani katika eneo lako la mamlaka. Tafadhali tazama hati ya Nyongeza ya sehemu ya 10 ili kupata maelezo zaidi kuhusu hili)
Unaweza kuondoa idhini yako ya Fomu ya Idhini ya Data za Bayometriki wakati wowote kwa kutumia Lango letu la Maombiau kichupo cha faragha kwenye Programu ya World. Tafadhali kumbuka kwamba ili kufuta nambari yako ya "thibitisho la kiumbe binafsi" (iris code), pia utafuta World ID yako kwenye lango hili: www.world.org/requestportal. |
Hauwezi kupatiana maelezo yako ya bayometriki kwenye kifaa cha Orb bila kusoma hati kamili na kutia sahihi fomu ya idhini. Hauwezi kupatiana maelezo yako ya bayometriki kwenye kifaa cha Orb ikiwa wewe ni mkaazi wa jimbo la Illinois, Texas, au Washington au mji wa Portland, jimboni Oregon au mji wa Baltimore, jimboni Maryland.
Tunafurahi kwamba umeamua kupanua ushiriki wako katika jamii ya World! World ni teknolojia huria, inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa ya watengenezaji maunzi tepe, watu binafsi, na wachangiaji wengine. Faragha ipo kwenye kiini msingi cha kampuni yetu. Tunatoa huduma ya kuthibitisha kuwe wewe ni kiumbe binafsi (Thibitisho la Mtu Binafsi Linalodumisha Faragha) kwa kupatiana data chache kadri iwezekanavyo. Pasi, hati rasmi hazihitajiki. Hata hatutaki kujua jina lako.
Asasi ya Worldcoin (“Asasi”, “sisi”, “yetu”, au “zetu”), ndio mhudumu anayeshughulikia teknolojia ya World. Uchakataji wetu (ukusanyaji, utumiaji, uhifadhi, ufichuaji, na ufutaji) wa data zako za kibinafsi unatawaliwa na hati mbili: Kauli ya Faraghana Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki. Kauli ya Faraghainasimamia data zinazokusanywa kupitia tovuti, programu, na huduma nyingine za Worldcoin, nayo Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki inaelezea jinsi tunavyochakata data zako za bayometriki zilizokusanywa kupitia kifaa chetu cha Orb. Hati hizi zinaendanisha moja kwa moja, na zote mbili ni muhimu katika kuelewa jinsi faragha yako inayoathiriwa na kushiriki katika mradi wa World. Kauli ya Faraghana Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki zimejumuishwa kwenye na kutawaliwa na Sheria na Masharti ya Mtumiaji.
Aidha, tuna faragha kama chaguomsingi na kimakusudi katika maeneo yote ya mamlaka ambako tunazidua World. Tunafanya tathmini za kina za mapema kwenye sheria za faragha za eneo husika kabla ya kuzindua na tunafanya juhudi zetu bora ili kuambatana na sheria za eneo husika hata ingawa World ni mradi wa kote ulimwenguni. Pia tutatumia tu data zako kwa malengo yaliyotajwa hapa chini katika Sehemu ya 2.2 (na Sehemu ya 3.4 ikiwa Umiliki Data unapatikana katika eneo lako la mamlaka na uuwezeshe), hata ikiwa sheria za faragha ya data nchini mwako hazingezuia jinsi tunavyotumia data zako.
Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki ina sehemu nne:
1. Historia kuhusu mradi wa World;
2. Idhini ya kuchakata data za bayometriki;
3. Kuwezesha Umiliki Data; na
4. Haki za mmiliki data.
1. Historia.
1.1 Mradi wa World.
World ni teknolojia huria, au mfumo, ulitengenezwa kumpa kila mtu uwezo wa kufikia uchumi wa kidijitali wa ulimwengu. Umebuniwa kuwa bila mamlaka kuu, kumaanisha kwamba hatimaye usimamizi wake na ufanyi maamuzi utakuwa juu ya jumuiya yeke ya kimataifa ua watumiaji. Cha muhimu, World, kupitia World ID, inaweza kuchukua jukumu muhimu katika kuonyesha utu kwa ulimwengu wa mtandaoni uliojaa artificial intelligence inayoendelea kuimarika. Uthibitishaji wa World ID ni wa bila malipo, wa faraghani na wazi kwa kila mwanadamu aliye na umri wa zaidi ya miaka 18.
1.2 Kifaa cha Orb.
Ili kutekeleza uthibitishaji salama, tumetengeneza kifaa cha kipekee kinachoitwa Orb. Kinathibitisha kwamba wewe ni “mwanadamu wa kipekee” bila kukuhitaji upatiane hati zozote za utambulisho au maelezo mengine kuhusu wewe ni nani. Orb inapiga picha kadhaa za ubora wa juu zaidi za macho yako (haswa, viini vya macho yako) na uso wako (kichwa chako na mabega yako).
1.3. Mdhibiti.
Sisi ndio Mdhibiti wa Data wa picha na data zako za bayometriki zilizokusanywa kupitia kifaa chetu cha Orb: Suite 3119, 9 Forum Lane, Camana Bay, PO Box 144, George Town, Grand Cayman KY1-9006, Cayman Islands. Asasi ya World inadumisha kituo kimoja katika Umoja wa Ulaya ili kuwezesha uchakataji huu wa data bila kutuma data kati kwenye Visiwa vya Cayman.
1.4 Idhini ya Kuchakata Data za Bayometriki.
Data tunazokusanya (imeelezewa hapa juu) zinaweza au zikakosa kuzingatiwa kuwa data za kibinafsi au data za bayometriki kulingana na sheria husika za unakoishi. Hata hivyo, ikija ni kwa usalama, tunazichukulia kama data za bayometriki na kuzishughulikia kwa usalama na uangalifu zaidi. Katika muktadha huu ni muhimu kufahamishwa kuhusu hatari za kuchakata data za kibayometriki. Tafadhali kumbuka kwamba yafuatayo ni maelezo ya hali ya juu kuhusu hatari zinazohusishwa na kuchakata data za bayometriki na si orodha kamili.
Data za bayometriki ni za kipekee kwako na haziwezi kubadilika. Hii inamaanisha kwamba ikiwa data za bayometriki zinaunganishwa na data zingine, data hizo zingine zinaweza kuhusishwa nawe vizuri sana. Ili kuzuia hili na kupunguza hatari hii, tunatumia “Zero Knowledge Proofs” kuhakikisha kwamba data zako za bayometriki hazihusishwi na akaunti yako ya Programu ya World, matumizi yako ya World ID na pochi lako la miamala.
Hatari fulani za bayometriki zinaweza kuwepo katika matukio yafuatayo ambayo tunajaribu kuzuia katika njia zifuatazo:
Data za bayometriki zinaweza kufichuliwa kutokana na shambulizi la udukuzi. Tunazuia hili kwa kutumia hatua za ulinzi wa mitambo za hali ya juu kuliko za kawaida.
Data za bayometriki zinaweza kuombwa na serikali. Tunazuia hii kwa kujitahidi sisi wenyewe kupinga maobi yoyote yasiyofaa na yasiyostahili kutoka kwa serikali.
Data za bayometriki zinaweza kutumiwa vibaya na mdhibiti data. Tunazuia hili kwa kufanya Asasi kujitahidi katika lengo lake lisilo la kifaida la mradi wa World katika makubaliano yake ya mkataba wa kuundwa.
2. Idhini ya Kuchakata Data za Bayometriki.
2.1 Data Tunazokusanya.
Kwa idhini yako, tunakusanya data zifuatazo za bayometriki na za kibinafsi kwa kutumia kifaa cha Orb:
Picha za viini vya macho yako na macho yako.Picha hizi zinapigwa kwa kutumia teknolojia ya “visible and near-infrared”. Kama ilivyobainishwa katika Sehemu ya 2.3, hapa chini, teknolojia hii si timilifu na huenda ikafanya makosa, kama vile kubaini kimakosa kwamba tayari umejisajili kwenye kifaa cha Orb.
Picha za uso wako.Picha hizi pia zinapigwa kwa kutumia teknolojia ya “visible”, “near-infrared”, na “far-infrared”. Pia tunapiga picha za kina (3D). Picha hizi zinatumika kuthibitisha kwamba wewe ni binadamu, na hivyo kusaidia kugundua na kuzuia ulaghai, na kufunza teknolojia ya kuzuia ulaghai (kwa pamoja picha hizi za uso na picha za viini vya macho hapa zinarejelewa kama “Data za Picha”).
Utohozi wa data zilizo hapa juu.Tunatumia teknolojia za hali ya juu na za kisasa zaidi pamoja na mtandao wetu wa “neural” ili kutengeneza uwakilisho wa tarakimu (“Utohozi”) wa picha zilizo hapa juu ili kuwezesha ulinganishaji wa mashine na utangamano baina yao. Utohozi huu ni msururu wa nambari (k.m, “10111011100…”) unaojumuisha vipengele muhimu zaidi vya picha. Haiwezekani kugeuza utohozi huu kikamilifu na kuwa picha asilia. Cha muhimu zaidi, tunatumia toleo lililobinafsishwa la Daugman Algorithm ili kutengeneza msururu huo wa nambari kutokana na picha ya kiini cha macho (“Iris Code”). Pia tunaondoa utambulisko kutoka kwenye Iris Code na kuwa vipande vya SMPC ili kuhakikisha kwamba watumiaji wanaweza kujisajilisjha mara moja pekee.
Muhimu!Tunakusanya Data za Picha ili kubaini kana kwamba wewe ni binadamu wa kipekee. Yaani, mfumo umebuniwa kuthibitisha kwamba wewe ni binadamu halisi (uhai) na kwamba hii ndio mara yako ya kwanza kutembelea kifaa cha Orb (upekee).Hatutumii data hizi ili kujuaweweni nani (utambulisho).
Tunaondoa utambulisho kwenye iris code yako kwa kuigawanya kwa vipande vidogo vinavyohifadhiwa na wahusika wanaoaminika katika teknolojia ya wahusika wengi. Maelezo zaidi kuhusu hii yanaweza kupatikana hapa: https://world.org/blog/announcements/worldcoin-foundation-unveils-new-smpc-system-deletes-old-iris-codes
Data tunazokusanya (imeelezewa hapa juu) zinaweza au zikakosa kuzingatiwa kuwa data za kibinafsi au data za bayometriki kulingana na sheria husika za unakoishi. Hata hivyo, ikija ni kwa usalama, tunazichukulia kama data za bayometriki na kuzishughulikia kwa usalama na uangalifu zaidi. Msingi wa kisheria wa kukusanya Data za Picha ni idhini yako ya moja kwa moja. Msingi wa kisheria wa kutengeneza utohozi wa Data za Picha (kama vile Iris Code) na kuondoa utambulisho wake ilo kuzilinganisha kwenye hifadhidata yetu ni idhini yako ya moja kwa moja.
2.2 Tunachofanya na Data Hizi.
Kwa idhini yako, tunatumia data zilizo hapa juu kwa malengo yafuatayo pekee (isipokuwa iwe umewezesha Umiliki Data, ulioelezewa hapa chini):
Kutathmini Iris Codes;
Kulinganisha Iris Code yako dhidi ya Iris Code zingine; na
Usalama na uzuiliaji ulaghai. Hii inajumuisha:
Kugundua kana kwamba mtumiaji ni binadamu aliyehai jambo linalojumuisha kukagua kana kwamba halijoto la nyuso zilizogunduliwa linalingana na halijoto la kawaida la mwili wa binadamu;
Kugundua kana kwamba usajili unaonyesha kiini cha jicho la binadamu halisi ambacho kimebadilishwa, kimegubikwa, jambo linalojumuisha kukagua kana kwamba uso unabadilika wakati wa usajili; na
Kugundua kana kwamba mtu husika amekuwa mbele ya kifaa cha Orb jambo linalojumuisha kuchakata Utohozi wa picha za uso uliohifadhiwa kwenye kifaa.
Tathmini zote za utohozi zinafanyika kwenye kifaa cha Orb.
Hatushiriki picha au utohozi wa picha hizo na mtu yeyote amabye hafanyi kazi kwenye mradi wa World na sio kwa malengo mengine kando na yaliyoelezewa hapa juu.
2.3 Usahihi.
Programu yetu inatumia uwezekano ili kubaini kana kwamba umejisajili kwenye kifaa cha Orb hapo awali. Si timilifu. Kwa hili, kinaweza kubainisha kimakosa kwamba tayari umejisajili kwenye kifaa cha Orb hapo awali. Kwa wakati huu, hatuna njia ya watumiaji kuripoti hitilafu zinazotuhumiwa au kupinga uamuzi wa teknolojia. Ukikubaliana na Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki, unatupatia idhini yako ya uamuzi huu otomatiki.
2.4 Si Lazima Uidhinishe Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki ili Kushiriki katika World.
Si lazima ukubaliane na Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki ili kushiriki katika World. Bado unaweza kuunda akaunti na kuwa na pochi la World bila kupatiana idhini hii, ingawa bado utahitajika kukubaliana na Sheria na Masharti ya Mtumiaji wa Worldna kusoma na kutambua Kauli yetu ya Faragha. Aidha, ukichagua kutokubaliana na Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki, basi hautaweza kushiriki katika vipengele fulani vya World, kama vile kuwa na Uthibitisho wa Mtu Binafsi wa kipekee na unaohamishika.
2.5 Kuondoa Idhini Yako
Unaweza kutekeleza haki zako kama mmiliki data ambazo zinaweza kujumuisha kuondoa idhini yako kwa kuwasiliana nasi kwenye:
Lango la Maombi la World, au kwa kututumia barua kwa anwani World Foundation, Suite 3119, 9 Forum Lane, Camana Bay, PO Box 144, George Town, Grand Cayman KY1-9006, Cayman Islands.
Ukiondoa idhini yako, basi hatutatumia tena data zako kwa malengo yaliyotajwa hapa juu, lakini matendo yote ya hapo mbeleni yaliyofanywa kwa kutumia idhini yako kabla ya kuiondoa yatasalia kuwa halali. Uchakataji ambao hautegemei idhini yako kama vile kuhifadhi Iris Code hauathiriwi na uondoaji idhini.
3. Kuwezesha Umiliki Data.
Tafadhali kumbuka kwamba Umiliki Data unaweza kuelemazwa katika baadhi ya maeneo ya mamlaka kwa ajili ya vigezo vya kiudhibiti.Tafadhali kagua sehemu ya hati za nyongeza ili kuthibitisha kama chaguo hili linakuhusu wewe.
3.1 Hali ya Sasa ya Mradi wa World
Ili kuimarisha usahihi wa mfumo kubaini ustahiki, tunahitaji kuendela kufunza programu ya teknolojia yetu. “Kufunza” kunamaanisha kutumia picha kutoka kwa watu halisia kama wewe ili kusaidia programu “kujifunza” kutofautisha wanadamu na wasio wanadamu na kutofautisha mtu moja kati ya watu wengine wote. Huku programu ikifunzwa na kuwa bora zaidi, tutaisasisha mara kwa mara. Hili linapofanyika, huenda tukahitaji kuthibitisha tena utambulisho wako wa kipekee wa kidijitali, jambo ambalo litahitaji kutumia Data za Picha zako tena.
3.2 Umiliki Data.
Ukiidhinisha Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki, katika Programu utaombwa, “Kuwezesha Umiliki Data.” Ukichagua kukubali Umiliki Data (kwa hiari), utaturuhusu:
Kuhifadhi Data za Picha na Utohozi zilizoandaliwa na kifaa cha Orb;
Kutuma Data za Picha kwa timu zetu zilizoko Umoja wa Ulaya na Marekani; na
Kutumia Data za Picha hizo kuendelea kutengeneza na kuimarisha programu, kama ilivyobainishwa hapa chini.
Kuweka lebo kwenye Data za Picha kwa kutumia jinsia, umri, na rangi ya ngozi ili kufunza teknolojia kuwa yenye usawa katika uanuai ulipo ulimwenguni.
Kuna uwezekano kwamba hii itakusaidia kuepuka baadhi ya usumbufu kwa sababu, ikiwa tuna Data za Picha zako, basi hautahitaji kurudi kwenye kifaa cha Orb ili kuthibitisha tena utambulisho wako wa kidijitali tunaposasisha programu. Pia itatusaidia kwa sababu tunaweza kutumia Data za Picha zako ili kufanya mfumo kuwa bora zaidi na kueneza World ulimwenguni kwa haraka zaidi. Kwa mara nyingine, si lazima Kuwezesha Umiliki Data, lakini kufanya hivyo kunaweza kukusaidia wewe pamoja nasi, na kwa hivyo tunashukuru sana.
3.3 Data Tunayokusanya Unapowezesha Umiliki Data.
Unapoidhinisha Fomu ya Idhini ya Data za Bayometriki, tunakusanya Data za Picha zako na picha za uso wako, kama ilivyobainishwa katika Sehemu ya II.1 hapa juu. Data za Picha tunazokusanya hazibadiliki ikiwa utakubaliana na Umiliki Data.
3.4 Tunachofanya na Data hizi Unapowezesha Umiliki Data.
Unapokubaliana na Fomu ya Idhini ya Data za Bayometriki, tunatumia data zilizo hapa juu kwa malengo yaliyobainishwa katika Sehemu ya 2.2. Pia unapowezesha Umiliki Data, tunatumia data hizi kwa malengo ya ziada yafuatayo:
Kusasisha Iris Code yako kwa njia otomatiki endapo tutasasisha teknolojia yetu inayotathmini Iris Code;
Kuimarisha na kuboresha tathmini za Iris Code na Utohozi;
Kuweka lebo kwenye data zilizokusanywa;
Kutumia data kufunza na kuchagua wahudumu wa kuweka lebo;
Kutengeneza na kufunza teknolojia ya kutambua, kuainisha na kutofautisha viini vya macho na nyuso za binadamu tofauti;
Kujaribu teknolojia dhidi ya matokeo yaliyowekewa lebo ya binadamu;
Kugundua na kuondoa kasoro kernyr teknolojia zetu (kama vile kufunza teknolojia kuwa yenye usawa kwa kutambua jinsia, umri, na rangi ya ngozi);
Kutengeneza, kufunza, na kujaribu mfumo wa kugundua kama mtumiaji ni binadamu na ana jicho halisi la binadamu na kama usajili ni halali;
Kutengeneza, kufunza, na kujaribu miigo inayotumia picha za viini vya macho vya kutengenezwa kwa ajili ya mafunzo zaidi ya teknolojia;
Kutengeneza, kufunza, na kujaribu miigo inayoimarisha utendakazi wa kifaa cha Orb na huduma kwa mtumiaji; na
Kufunza na kukutathmini wafanyakazi wanafanya kazi kwa kutumia mifumo hii.
Hatutawahi kuuza data zako. Pia hatutatumia data zozote zilizoorodheshwa kwenye fomu hii ili kufuatilia mienendo yako au ili kukutangazia bidhaa za wahusika wengine.
4. Tunaosambazia Data
Wakati ambapo tunasambaza data zako nje ya shirika letu, kila wakati:
Tunazisambaza kwa njia salama;
Kuchukua hatua kuhakikisha kwamba inashughulikiwa kwa njia ambayo inaendanisha na jitihada zetu kwa faragha yako; na
Tunazuia kampuni zingine kutozitumia kwa malengo yao binafsi.
Tunasambazai data zako kwa njia hizi chache:
Kwa Tools for Humanity:Tunafichua tu data kwa watoa huduma kwetu, Tools for Humanity, na wanatimu wao ambao wanahitaji kuzifikia ili kuweza kufanya kazi na majukumu yao. Tunafichua tu kiwango cha data ambacho kinahitajika ili kufanya kazi na majukumu fulani na kuwa na mfumo ulio na udhibiti mkali wa ufikiaji.
5. Utumaji Data, pamoja na hatari Zinazoweza Kuwepo.
Unapowezesha Umiliki Data, na hivyo kutuidhinisha na kutykubalisha kutumia data zako kwa malengo yaliyoelezewa hapa juu katika Sehemu ya 3.4, kwa ujumla tunatuma data hizo kwa timu zetu za Utafiti na Utengenezaji (Research and Development, “R&D”), na hii inaweza kupelekea data zako kutumwa nje ya nchi ambako data hizo zilikusanywa. Timu hizi kwa sasa ziko katika Umoja wa Ulaya na Marekani. Kauli yetu ya Faraghainaelezea jinsi tunavyolinda na kuambatana na sheria za utumaji data nje ya nchi. Sehemu ya 6 ya Kauli ya Faraghaimebainisha hatari zinazohusiana na utumaji huo wa data nje ya nchi.
Kwa idhini yako tunahifadhi Data za Picha katika vikapu vya kikanda vilivyo EU, Marekani, Brazili, India, Singapoo, na Afrika Kusini. Ukijisajili katika maeneo haya mamlaka data zako zitahifadhiwa huko. Ukijisajili katika nchi nyingine Data za Picha zako zitahifadhiwa katika mojawapo ya vikapu hivyo kulingana na kasi na upatikanaji wa mtandao husika. Kwa mfano:
Ukijisajili ukiwa EEA, Uswizi au Uingereza, basi Data za Picha zako zitahifadhiwa katika EU.
Ukijisajili ukiwa nchini Kenya, Uganda, Ghana, au Naijeria, basi Data za Picha zako zitahifadhiwa nchini South Africa au katika EU, kulingana na kasi ya mtandao wakati unapojisajili.
Ukijisajili ukiwa nchini Indonesia, basi Data za Picha zako zitahifadhiwa nchini Singapoo au India, kulingana na kasi ya mtandao wakati unapojisajili.
Ukijisajili ukiwa nchini Meksikoa, basi Data za Picha zako zitahifadhiwa nchini Marekani au Brazili, kulingana na kasi ya mtandao wakati unapojisajili.
Ukijisajili ukiwa nchini Chile, Ajentina, au Kolombia, basi Data za Picha zako zitahifadhiwa nchini Brazili.
Kwa madhumuni ya Ufunzaji Mashine Data zote za Picha kisha zitatumwa na kuhifadhiwa katika Umoja wa Ulaya na Marekani.
Hapa chini ni orodha ya hatari zinazoweza kutokea tunapotuma data zako hadi Marekani, Umoja wa ulaya, au nchini nyingine. Hapa chini pia tumeweka muhtasari wa jinsi ya kuzuia hatari husika.
Tunapofanya kadri tuwezayo ili kuhakikisha kwamba wachakataji (yaani “wanakandarasi wadogo”) wetu wana jukumu la kimkataba la kulinda data zako vya kutosha, wanakandarasi hawa wadogo huenda wasiwe chini ya sheria za faragha ya data za nchi yako. Wakandarasi wakichakata data zako kwa njia isiyo ya kisheria bila idhini, basi huenda ikawa vigumu kudai haki zako za faragha dhidi ya wakandarasi hao. Tunazuia hatari hii kwa kuwa na makubaliano dhabiti ya uchakataji data na wakandarasi wetu ambayo inawabidi kulinda data kwa kiwango sawa na cha GDPR na kutimiza maombi ya wahusika.
Kuna uwezekano kwamba sheria ya faragha ya data nchini mwako haiendanishi na sheria za faragha ya data nchini Marekani, au katika EU. Daima tutajaribu kuambatana na kiwango cha juu zaidi cha ulindaji data ambacho tunatumia. Kufikia sasa, tumepata kwamba GDPR inatimizi hitaji hili na tunachukulia data zote ni kama zinatawaliwa na GDPR.
Kuna uwezekano kwamba data zako zitaweza kufikia na maafisa au mamlaka za kiserikali. Katika matukio hayo tumejitayarisha kupinga mahakamani ombi lolote la kiserikali la kufikia data ambalo si halali, linapita mipaka, au si la kisheria. Aidha tunatumia usimbaji wa hali ya juu ili kuzuia ufikiaji bila idhini.
Tafadhali kumbuka kwamba orodha hii ina mifano, lakini huenda haijajumuisha hatari zote zinazoweza kuwepo.
Hatutauza, kukodisha, kufanya biashara, au vinginevyo kufaidika kutokana na data zako za bayometriki.
6. Uhifadhi Data.
Ukikosa kukubali Umiliki Data, tutafiuta data za picha zako muda mfupi baada ya kujisajili. Hatua sawa inachukuliwa kwenye Fungu la Data unaloweza kupakua kwa Umiliki wa Kibinafsi. Iris Codes zinahifadhiwa tu kwa njia ambayo zimeondolewa utambulisho. Watumiaji wanaweza kutekeleza haki zao katika lango hili: https://world.org/requestportal. Yafuatayo yanatumika tu kwa watumiaji wa Umiliki Data: Tutahifadhi Data za Picha za Umiliki Data mpaka tamatisho la utengenezaji na uboreshaji wa teknolojia au kama inavyohitajika na sheria au kanuni. Lakini, tutafuta Data za Picha baada ya wewe kutuma ombi. Aidha, tunaahidi kufuta Data zote za Picha baada ya upeo wa miaka kumi baada ya kukusanywa bila kujali maendeleo ya teknolojia na kuna uwezekano kwamba ufutaji husiani wa Data zote za Picha utakamilishwa mapema zaidi.
7. Umiliki wa KIbinafsi na Uidhinishaji Tena (kulingana na upatikanaji katika maeneo yaliyochaguliwa ya mamlaka)
Pale ambapo umiliki wa kibinafsi unapatikana, tunatuma picha za uso wako na macho yako na utohozi wowote ulioandaliwa na kifaa cha Orb (Fungu la Data) hadi kwenye simu yako kwa njia ya usimbaji wa mwisho-hadi-mwisho (hii inamaanisha hatuwezi kusoma data hizo).
Tunafuta kabisa Fungu la Data (kando na Iris Code) kutoka kwenye mifumo yetu baada ya kutuma Fungu la Data kwenye simu yako (angalau tufute data hizi baada ya mwezi mmoja katika matukio ambapo k.m. upakuaji haukufaulu). Kwa Umiliki wa Kibinafsi, tunachakata data zifuatazo kwa malengo yafuatayo:
Picha ya uso wako inapigwa kwa kutumia simu yako (selfie) na kubadilishwa kuwa Utohozi (Kiolezo cha Uso). Kiolezo hii cha Uso kilichobuniwa kwa ulinganishaji wa 1:1 kinakuwezesha kuthibitisha kwamba wewe ndiye mmliki halisi wa World ID ambayo inaweza kuhitajika katika naadhi ya matumizi ya World ID katika siku zijazo. Hii inaweza kuzuia mtu mwingine kutumia World ID yako. Utaombwa idhini yako kila mara kabla ya uidhinishaji huo wa uso kufanyika.
Kukuwezesha kujiunga kwenye Umiliki Data na hata vipengele vingine, ambapo data zako zitatumwa kwenye seva au hifadhidata ukichagua kufanya hivyo. Utaombwa idhini yako kabla kujiunga na Umiliki Data huo kufanyika.
8. Tathmini za Athari ya Usalama wa Data na Ulinzi wa Data
Tumefanya tathmini ya athari ya ulinzi wa data unaotamatisha kwamba uchakataji wa data inafaa na unahitajika. Matokeo makuu na muhtasari wa hati hii zinaweza kupatikana zikiwa zimechapishwa hapa. Data za kibinafsi zimelindwa kwa hatua zifuatazo:
Uthibitishaji wa hatua kadhaa kwa huduma zote katika muundombinu wa IT wa ndani
Uhamishaji wa TLS, usimbaji tulivu, ngazi za pili za usimbaji, funguo za kusimbua kuhifadhiwa kwenye maunzigumu tofauti.
Tunatenganisha data za bayometriki na data nyingine za mtumiaji, seva tofauti (hata akaunti tofauti za AWS), viungo kati ya hifadhidata vinaondolewa kila wakati.
Ni lazima kurekodi shughuli zote za ndani kwenye seva zinazohifadhi data za bayometriki, shughuli zozote zisizo za kawaida zinatambuliwa mara moja.
Udhibiti wa haki ya ufikiaji na uondoaji haki ya ufikiaji (ufikiaji inapohitajika pekee)
Sera ya ndani ya uchakataji data za bayometriki imebuniwa kulingana na sera ya bayometriki ya Msalaba Mwekundu (Red Cross).
9. Haki Zako
Kulingana na eneo lako la mamlaka, kwa kawaida una haki fulani kuhusiana na data zako. Tafadhali soma maelezo yaliyo hapa chini pamoja na sehemu yahati za nyongezaili kujua haki ulizo nazo kulingana na eneo lako la mamlaka.
Haki hizi zinatumika pale tu ambapo tunaweza kumtambulisha mwombaji katika hifadhidata yetu na pale tu ambapo hatukiuki haki zingine za mmiliki data kwa kutekeleza haki za mwombaji:
Una haki ya kupata kutoka kwetu wakati wowote baada ya kutuma ombi maelezo kuhusu data za kibinafsi tunazochakata kukuhusu. Una haki ya kupata kutoka kwetu data za kibinafsi zinazokuhusu.
Una haki ya kuagiza kwamba mara moja tusahihishe data za kibinafsi zinazokuhusu ikiwa si sahihi.
Una haki ya kuagiza kwamba tufute data za kibinafsi zinazokuhusu. Mahitaji haya yanaonyesha haki ya kufutwa ikiwa data za kibinafsi si muhimu tena kwa madhumuni ambayo ilifanya zikusanywe au kuchakatwa, mradi mahitaji ya kufuta chini ya sheria husika yamebainishwa (k.m. sheria kadhaa za maeneo ya mamlaka zinatuhitaji kuhifadhi maelezo ya miamala kwa kipindi fulani cha muda)
Una haki ya kuondoa kwa hiari idhini yako ya uchakataji wowote wa data kwa idhini au kukataa uchakataji wa data ikiwa si kwa idhini.
10. Hati za Nyongeza
Ifuatayo, hati kadhaa za nyongeza zinatoa maelezo yanahitajika kisheria kwa masoko husika ambapo tunaendesha shughuli. Maelezo haya ni sehemu ya idhini kulingana na eneo ambako mmiliki data anaishi. Maelezo haya yanaweza kutofautiana na maelezo ya eneo lako kwa sababu tunazuilia huduma fulani katika maeneo fulani ya mamlaka. Endapo kuna tofauti na yaliyo hapa juu kauli maalum iliyo hapa chini kuhusu eneo fulani la mamlaka inatumika:
Tafadhali kumbuka kwamba marejeleo ya eneo maalum la mamlaka haimaanishi teknolojia ya World tayari inapatikana katika eneo hilo la mamlaka, hakuna marejeleo kama hayo yanatoa hakikisho zozote kwamba itapatikana hivi punde. Ujumuishaji maeneo maalum ya mamlaka ni sehemu ya tathmini endelevu ya kina ya kisheria ya World ya maeneo tofauti ya mamlaka kote ulimwenguni na itahitimu kama kazi inayoendelea.
NYONGEZA YA A: ENEO LA KIUCHUMI LA ULAYA NA UINGEREZA
Ikiwa upo katika EEA au Uingereza (“UK”) yafuatayo yanatumika kwako:
Chaguo la Umiliki Data:ipo
Kipengele cha Umiliki wa Kibinafsi:ipo baada ya kutangazwa na kuzinduliwa.
Una angalau haki zifuatazo. Ili kutumia haki zako zinazopatikana chini ya GDPR, tafadhali wasiliana nasi kwenye Lango letu la Maombi. Kando na matukio ya kipekee, tutajibu ombi lako ndani ya makataa ya kisheria ya mwezi mmoja. Matumizi ya neno GDPR katika sehemu ifuatayo pia inajumuisha UK-GDPR. Matumizi ya neno GDPR katika sehemu ifuatayo pia yanajumuisha UK-GDPR iliyojumuishwa katika sheria za kitaifa za Uingereza kama Sheria ya UK ya Ulinzi wa Data ya 2018 na kuhifadhiwa kama sehemu ya sheria za Uingereza na Wales, Scotilandi na Ayalandi Kaskazini kwa Sehemu ya 3ya sheria ya European Union (Withdrawal) Act 2018 na kama ilivyorekebishwa na Schedule 1kwenye Data Protection, Privacy and Electronic Communications (Amendments etc) (EU Exit) Regulations 2019 (SI 2019/419).
Una haki ya kupata kutoka kwetu wakati wowote baada ya kutuma ombi maelezo kuhusu data za kibinafsi tunazochakata kuhusiana na ndani ya wigo wa Kifungu cha 15 cha GDPR.
Una haki ya kuagiza kwamba mara moja tusahihishe data za kibinafsi zinazokuhusu ikiwa si sahihi.
Una haki, chini ya hali zilizoelezewa katika Kifungu cha 17 cha GDPR, kuagiza kwamba tufute data za kibinafsi zinazokuhusu. Mahitaji haya yanaonyesha haki ya kufutwa ikiwa data za kibinafsi si muhimu tena kwa madhumuni ambao ilifanya zikusanywe au kuchakatwa, na pia katika matukio ya uchakataji usio wa kisheria, uwepo wa pingamizi au uwepo wa jukumu la kufuta chini ya sheria la Umoja au sheria ya Jimbo kwa ambayo tupo chini yake.
Una haki ya kuagiza kwamba tuwekee vikwazo uchakataji kulingana na Kifungu cha 18 cha GDPR.
Una haki ya kupokea kutoka kwetu data za kibinafsi zinazokuhusu ambazo umetupatia kwa umbizo sambamba, linalotumika kwa kawaida, na linalosomeka na mashine kulingana na Kifungu cha 20 cha GDPR.
Wakati wowote, kwa misingi inayohusiana na hali yako haswa, una haki ya kupinga uchakataji wa data za kibinafsi zinazokuhusu ambao umefanywa, na kadhalika, kwa misingi ya Kifungu cha 6 (1) sentensi ya 1, eneo la f kwenye GDPR, kulingana na Kifungu cha 21 cha GDPR.
Una haki ya kuwasiliana na mamlaka adilifu ya usimamizi endapo kutakuwa na malalamishi kuhusu uchakataji data unaofanywa na mdhibiti. Mamlaka ya usimamizi inayowajibika ni: the Bavarian State Office for Data Protection Supervision (Bayerisches Landesamt für Datenschutz). Nchini UK mamlaka adilifu ya usimamizi ni Ofisi ya Kamishna wa Maelezo (Information Commissioner’s Office, ICO).
Ikiwa uchakataji wa data za kibinafsi unategemea idhini yako, una haki chini ya Kifungu cha 7 cha GDPR una haki ya kughairi idhini yako ya matumizi ya data zako za kibinafsi wakati wowote katika siku zijazo, ambapo kughairi huku ni rahisi kufanya kama ilivyo kuwa rahisi kupatiana idhini. Tafadhali kumbuka kwamba kughairi kunaathiri tu siki zijazo. Uchakataji uliofanyika kabla ya kughairi hauathiriki.
NYONGEZA YA B: JAPANI
Ikiwa unaishi Japani, aidha, yafuatayo yanatumika kwako:
Baada ya kuchakata data zako za bayometriki ili kuandaa Iris Code hatuchakati data zozote zingine za kibinafsi kutokana na mchakato wa kifaa cha Orb.
Chaguo la Umiliki Data:ipo
Kipengele cha Umiliki wa Kibinafsi:ipo.
B1: Maelezo Kuhusiana na Kanuni za Japani
Tunaambatana na sheria na kanuni za Japani, pamoja na Sheria ya Japani ya Ulinzi wa Maelezo ya Kibinafsi (Act on the Protection of Personal Information, “APPI”). Sehemu hii inatumika katika jinsi tunavyoshughulikia “maelezo ya kibinafsi” kama ilivyobainishwa katika APPI kwa pamoja na sehemu nyingine za Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki
B2: Kusambaza Data
Bila kujali Sehemu ya 4 ya Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki, isipokuwa iwe imeruhusiwa vinginevyo na sheria husika, hatufichui, kuuza, kupatiana, kusambaza, wala kutuma maelezo yako ya kibinafsi kwa mhusika yeyote mwingine.
B3: Hatua za Udhibiti wa Kiusalama
Kulingana na Sehemu ya 6 hadi Sehemu ya 8 ya Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki, tunachukua hatua hitajika na mwafaka ili kuzuia uvujaji, au upotezaji, au uharibifu wa maelezo yako ya kibinafsi yanayoshughulikiwa, na pia kudumisha usalama wa maelezo ya kibinafsi, kama vile kwa kuweka sheria za kushughulikia maelezo ya kibinafsi, ufuatiliaji wa mara kwa mara, mafunzo ya mara kwa mara kwa waajiriwa katika kushughulikia maelezo ya kibinafsi, uzuiaji wizi au upotezaji wa vifaa vinavyotumika kushughulikia maelezo ya kibinafsi, na utekelezaji wa vidhibiti vya ufikiaji. Pia tunazimamia ipasavyo wanakandarasi na waajiriwa wetu wanaoshughulikia maelezo ya kibinafsi. Unaweza kupata maelezo ya ziada kuhusu hatua za kudhibiti usalama zilizowekwa kuhusiana na kushughuikia maelezo yako ya kibinafsi kwa kuwasiliana nasi kwenye Lango letu la Maombi.
B4: Haki za Kisheria chini ya APPI
Ili kutumia haki zako zinazopatikana chini ya APPI tafadhali wasiliana nasi kwenye Lango letu la Maombi
NYONGEZA YA C: AJENTINA
Ikiwa makazi yako ni Jamhuri ya Ajentina, yafuatayo yanatumika kwako:
Chaguo la Umiliki Data:ipo
Kipengele cha Umiliki wa Kibinafsi:ipo baada ya kutangazwa na kuzinduliwa.
Tunakufahamisha kwamba SHIRIKA LA UFIKIAJI WA MAELEZO YA HADHARANI, kwa uwezo wake kama Shirika la Udhibiti la Sheria Na. 25,326, lina mamlaka ya kusikia malalamishi na madai yaliyoandikishwa na wale ambao haki zao zimeathiriwa na kukosa kuambatana na sheria zilizowekwa kuhusiana na ulinzi wa data za kibinafsi.
Shirika hili linaweka kufikiwa kama ifuatavyo:
Anwani: Av. Pte. Gral. Julio A. Roca 710, 5th floor - Autonomous City of Buenos Aires
Postal Code: C1067ABP
Nambari ya simu: (54-11) 3988-3968
Barua pepe: [email protected]
NYONGEZA YA D: SINGAPOO
Ikiwa wewe ni mkaazi wa Singapoo yafuatayo yanatumika kwako:
Chaguo la Umiliki Data:ipo
Kipengele cha Umiliki wa Kibinafsi:ipo baada ya kutangazwa na kuzinduliwa.
D1. Ukusanyaji, matumizi na ufichuaji wa data zako za kibinafsi
Ikiwa wewe ni mkaazi wa Singapoo na kwa idhini yako, tutakusanya, kutumia na vinginevyo kufichua data zako za kibinafsi kwa ajili ya kila moja ya malengo yaliyobainishwa kwenye kauli yetu ya faragha. Unaweza kutumia haki yako ya kuondoa idhini yako wakati wowote, lakini tafadhali kumbuka kwamba huenda tunashindwa kuendelea kukupa huduma zetu kulingana na hali na wigo wa ombi lako. Tafadhali pia kumbuka kwamba kuondoa idhini hakuathiri haki yetu ya kuendelea kukusanya, kutumia na kufichua data za kibinafsi pale ambapo ukusanyaji, matumizi na ufichuaji huo bila idhini unaruhusiwa au unahitajika chini ya sheria husika.
D2. Kutumia haki zako kama mmiliki data
Unaweza kudhibiti data za kibinafsi ambazo tumekusanya na kutumia haki zozote kwa kuwasiliana nasi kwenye Lango letu la Maombi. Tunalenga kujibu ombi lako punde iwezekanavyo, kwa kawaida ndani ya siku 30. Tutakufahamisha mapema ikiwa hatujaweza kujibu ombi lako ndani ya siku 30, au ikiwa hatuwezi kutimiza ombi lako na sababu kwa nini.
Inaporuhusiwa na sheria, tunaweza kukutoza ada ya kiutawala ili kutimiza ombi lako.
D3. Kutuma data zako za kibinafsi hadi nchi zingine
Ikiwa wewe ni mkaazi wa Singapoo na tumekusanya data zako, tunaweza pia kutuma data zako nje ya Singapoo mara kwa mara. Hata hivyo, kila wakati tutahakikisha data zako za kibinafsi zinaendelea kupokea kiwango cha ulinzi ambacho kinafanana na ulinzi unaotolewa na Sheria ya Singapoo ya Ulinzi wa Data za Kibinafsi ya 2012, [kama vile kupitia matumizi ya ASEAN Model Contractual Clauses].
NYONGEZA YA E – KOREA KUSINI
Ikiwa wewe ni mkaazi wa Korea Kusini, yafuatayo yanatumika kwako.
Iris Code zinazingatiwa kuwa data bila jina chini ya sheria za Korea Kusini. Baada ya kuchakata data zako za bayometriki -(ambazo haziondoki kwenye kifaa cha Orb) ili kuandaa Iris Code hatufikii wala kuchakata data zozote zingine za kibinafsi kutoka kwenye kifaa cha Orb.
Chaguo la Umiliki Data:haipo
Kipengele cha Umiliki wa Kibinafsi:haipo.
NYONGEZA YA F - BRAZILI
Ikiwa unaishi nchini Brazili, ikiwa data zako za kibinafsi zilizkusanywa nchini Brazili, au ikiwa unatumia Huduma zetu nchini Brazili, ifuatayo inatumika kwako.
Iris Code zinazingatiwa kuwa data bila utambulisho chini ya Sheria No. 13,709/2018 (Sheria Jumla ya Ulinzi wa Data, au “LGPD”). Baada ya kuchakata data zako za bayometriki ili kuandaa Iris Code hatuchakati tena data zingine zozote za kibinafsi kutokana kwenye kifaa cha Orb.
Chaguo la Umiliki Data:ipo
Kipengele cha Umiliki wa Kibinafsi:ipo baada ya kutangazwa na kuzinduliwa.
F1. Data za Bayometriki
Chini ya LGPD, daya za bayometriki zinazingatiwa kuwa maelezo nyeti ya kibinafsi. Tutachakata tu data hizi ukitupatia idhini maalum ya malengo yaliyobainishwa vizuri. Katika hali fulani, tunaweza kuchakata data zako za bayometriki bila idhini yako wakati kwa kweli inahitajika, kama vile ili kutii makujumu ya kisheria au kiudhibiti, kutekeleza haki zetu (ikijumuisha kwenye mikataba na kesi za kisheria), au ili kuzuia ulaghai na kulinda uadilifu wa mmiliki data.
Tunatumia hatua na mbinu za kiusalama za hali ya juu ili kulinda maelezo yako ya kibinafsi, pamoja na usimbaji na uondoaji utambulisho ili kuhakikisha kwamba data zako nyeti yanalindwa na hayawezi kuhusishwa na mtu binafsi, kulingana na hali.
Pia tunakadiria data, na kuunganisha makundi makubwa ya data ili kuondoa vitambuaji binafsi au marejeleo kwa mtu yeyote binafsi. Tunatumia data bila utambulisho au zilizokadiriwa kwa madhumuni yetu ya kibiashara, kama vile kutusaidia kuelewa mahitaji na tabia za watumiaji, kuimarisha huduma zetu, kufanya shughuli za umaizi na uuzaji wa kibiashara. kugundua hatari za kiusalama, na kufunza teknolojia zetu. Pia tunachakata data zako za bayometriki iki kuhifadhi maelezo yako ya kibinafsi, kuthibitisha, na kutengeneza Iris Code.
Tutatumia tu data zako za bayometriki kwa malengo yaliyotajwa hapa juu ukitupatia idhini maalum kupitia Fomu hii ya Idhini ya Dataza Bayometriki.
Kwa kuchagua Umiliki wa Kibinafsi au Umiliki Data, kama ilivyobainishwa kwenye Fomu hii ya Idhini ya Data za Bayometriki, data zako za bayometriki zitahifadhiwa kwenye kifaa chako. Hapa, ni lazima utumie kinga za ziada ili kuhakikisha usalama wa data zako za bayometriki zilizohofadhiwa kwenye kifaa chako, kwani hatuna uwezo wa kufikia au kudhibiti mfumo wa hifadhi ya kifaa chako nje ya Programu ya World
F.2 Kutuma Data Zako za Kibinafsi Kimataifa
Ikiwa LGPD inatumika kwako, na tumekusanya data zako za kibinafsi, tunaweza pia kuzituma nje ya nchi. Hata hivyo, kila wakati tutahakikisha kwamba data zako za kibinafsi zinatumwa tu hadi nchi za kigeni aukwa mashirika ya kimataifa ambayo yana kiwango cha ulinzi ambacho ni sawa na cha LGPD, kama inavyotambuliwa katika maamuzi ya kutosha uanayotolewa na ANPD. Endapo hakutakuwa na uamuzi kuhusu kutosha, tutaendelea kufuata kiwango cha ulinzi ambacho angalau ni sawa na kinachotolewa na LGPD kwa kutumia Vifungu vya Kimkataba vilivyowekwa katika kanuni za ANPD au tunapopokea idhini yako maalum ya kutuma kimataifa.
WFDCF20241112