Terms, Privacy and Data

  • Sheria na Masharti ya Asasi ya World Foundation

  • Ilani ya Faragha ya Asasi ya World

  • Sera ya Kuki ya Asasi ya World Foundation

  • Fomu ya Idhini ya Dataza Bayometriki ya World Foundation

  • Kanusho la Ruzuku ya Pamoja ya Binadamu

  • Aviso de Privacidad de Worldcoin Foundation - Argentina

  • Foundation Data Processing Agreement

Sera ya Kuki ya Asasi ya Worldcoin

Effective January 10 2025

Sera ya Kuki ya Asasi ya Worldcoin

Sera hii ya Kuki inaelezea jinsi sisi, Asasi ya Worldcoin (kwa pamoja “sisi” au “Asasi”), tunavyotumia kuki na teknolojia sawa, kama vile web beacons, ili kufuatilia mienendo ya mtandaoni ya watumaiji wetu wanapotembelea tovuti zetu na Huduma nyingine. Web beacon ni mbinu inayotumika kwenye kurasa za tovuti bila kuzuiwa kuruhusu (kawaida kwa njia isiyoonekana) kuangalia kwamba mtumiaji ametembelea maudhui fulani. Sera hii ya Faragha imejumuishwa na ipo chini ya Ilani ya Faragha ya Asasi ya Worldcoin.

Kulingana na ni tovuti ipi kati ya tovuti zetu (worldcoin.org, developer.worldcoin.org, na docs.worldcoin.org) unayotembelea, tunatumia kuki tofauti. Tunanatumia mbinu za majina ya misimbo kwa kuki zote ili kuhakikisha faragha ya mtumiaji.

Tunatumia aina zifuatazo za kuki:

Kuki Muhimu Sana:Kuki hizi ni muhimu ili Huduma zifanye kazi na haziwezi kuzimwa katika mifumo yako. Kwa kawaida huwa zimepangwa kutenda kulingana na hatua unazochukua ambazo zinajumuisha kuomba huduma, kama vile kuingia kwenye akaunti au kujaza fomu. Hivi pia vinajumuisha kuki tunazoweza kutegemea kuzuia ulaghai. Unaweza kuandaa kivinjari chako kuzuia au kukupasha habari kuhusu kuki hizi, ila baadhi ya Huduma huenda zikakosa kufanya kazi. Misingi ya kisheria ya kutumia Kuki Muhimu Kabisa ni haja halali. Haja halali inayoangaziwa ni kutoa taarifa bila malipo mtandaoni kwa watu ambao wanaamua kwa njia huru kutembelea tovuti hiyo ambayo haingeweza kufanya kazi bila Kuki Muhimu Kabisa.

Kuki za Utendakazi/Uchambuzi: Kuki hizi zinatuwezesha kuhesabu mara ya kutembelea na vyanzo vya trafiki ili tuweze kupima na kuimarisha utendakazi wa Huduma zetu. ZInatusaidia kujua umaarufu wa ukurasa na harakati za wageni kuhusu Huduma. Maelezo yote yanayokusanywa na kuki hizi yamekadiriwa na kwa hivyo hayana utambulisho. Ukikosa kuruhusu kuki hizi, hatutajua wakati umetumia Huduma zetu, na hatutaweza kufuatilia utendakazi wake. Misingi ya kisheria ya kutumia Kuki za Utendakazi/Uchambuzi ni idhini ya mtumiaji. Ridhaa yako inaweza kuondolewa kwa hiari wakati wowote.

Kuki za Utendakazi: Kuki hizi zinatuwezesha kukumbuka machaguo uliyofanya na kubinafsisha Huduma zetu ili tuweze kukupa maudhui muhimu. Kwa mfano, kuki ya utendaji inaweza kukumbuka mapendeleo yako (k.m. chaguo la nchi au lugha), au jina lako la mtumiaji. Msingi wa kisheria wa matumizi ya Kuki za Utendakazi ni idhini ya mtumiaji. Ridhaa yako inaweza kuondolewa kwa hiari wakati wowote.

Hii ni orodha ya kuki tunazotumia kwenye sehemu tofauti za tovuti:

Tovuti

Kuki zinazotumika

worldcoin.org

Kwenye tovuti ya worldcoin.org tunatumia Kuki Muhimu Kabisa na Kuki za Utendakazi/Uchambuzi za hiari (kuki moja kutoka kwenye kila kategoria). Tunatumia tu uchambuzi ili kuboresha bidhaa yetu. Hatutumii data zako ili kuziuza kwa ajili ya kufanya matangazo ya wahusika wengine.

developer.worldcoin.org

Kwenye lango la Worldcoin Developer Portal tunatumia Kuki Muhimu Kabisa na Kuki za Utendakazi/Uchambuzi za hiari (kuki moja kutoka kwenye kila kategoria). Tunatumia tu uchambuzi ili kuboresha bidhaa yetu. Hatutumii data zako ili kuziuza kwa ajili ya kufanya matangazo ya wahusika wengine.

docs.worldcoin.org

Kwenye lango la Worldcoin Documentation tunatumia tu Kuki ya Utendakazi/Uchambuzi ya hiari ili kuripoti bila kujitambulisha chambuzi zinazotusaidia kuboresha bidhaa yetu. Hatutumii data zako ili kuziuza kwa ajili ya kufanya matangazo ya wahusika wengine.

Sisi na watoa huduma wengine tunatumia viashiria vya tovuti (web beacons) kwa sababu zilizoorodheshwa hapa chini, lakini kimsingi ni kutusaidia kudhibiti maudhui kwa njia bora kuhusu Huduma zetu kwa kutufahamisha ni maudhui gani yanayoleta ufanisi.

Kwa pamoja, zana hizi zinatuwezesha:

  • Kufanya chambuzi za tovuti;
  • Kuzuia ulaghai na kuzuia mashambulizi dhidi ya tovuti na Huduma zetu; na

Tunatumia kuki na vifuatiliaji ili kukupa kitambulisho cha kipekee ili tuweze kurekodi:

  • Tovuti unazotembelea
  • Anwani yako ya IP

Unaweza kuzuia kuki wakati wowote kwa kutumia mipangilio ya kivinjari chako, lakini kufanya hivyo huenda kukawekea vikwazo huduma yako ya kuvinjari na uwezo wako wa kutumia vipengele fulani vya Huduma.

JE, KUKI ZITADUMU KWA MUDA GANI KWENYE KIVINJARI CHANGU?

Urefu wa muda ambao kuki itakuwa kwenye kivinjari chako utategemea kama ni kuki ya “kudumu” au ya “muda”. Kuki za muda zitakuwa kwenye kifaa chako hadi utakapofunga kivinjari chako. Kuki za kudumu zinakuwa kwenye kifaa chako cha kuvinjari hadi zitakapoishiwa na muda au zitakapofutwa.

JINSI YA KUDHIBITI KUKI NA TEKNOLOJIA ZA AINA HIYO

Una haki ya kuamua ikiwa utakubali kuki ambazo si Kuki Muhimu Kabisa.

Unaweza pia kuchagua jinsi kuki (katika tovuti zote) zinashughulikiwa kwenye kifaa chako kupitia mipangilio ya kivinjari chako ikiwemo kuzuia au kufuta kuki zote au kuki za wahusika wengine tu. Kila mtengenezaji wa kivinjari fulani ni tofauti, kwa hivyo angalia kwenye menyu ya “Help” (msaada) ya kivinjari chako ili kujifunza jinzi ya kubadilisha mapendeleo yako kuhusu kuki.

Zaidi ya hayo, mitandao mingi ya matangazo inakupa njia ya kuchagua kuondoka kwenye matangazo lengwa. Ikiwa ungependa kupata maelezo zaidi, tafadhali tembelea aboutads.info/choices/ au youronlinechoices.com.

Do Not Track (Usifuatilie): Baadhi ya vivinjari vya tovuti - kama vile Internet Explorer, Firefox, na Safari - vinajumuisha uwezo wa kuwasilisha ishara za "Do Not Track" au “DNT”. Kwa kuwa viwango vya kawaida vya isahara za "DNT" havijawekwa, tovuti zetu kwa sasa hazichakati au kutangamana na ishara za “DNT”.



JE, SERA HII YA KUKI ITASASISHWA?

Tunaweza kubadilisha sera hii ya kuki mara kwa mara ili kuonyesha, kwa mfano, mabadiliko kwenye kuki tunazotumia au kwa sababu nyinginezo za kiutendakazi, kisheria au kiudhibiti. Tukifanya masasisho yoyote, utajulishwa unapotembelea tovuti yetu kwa mara ya kwanza baada ya mabadiliko hayo. Unaweza pia kurejelea ukurasa huu ikiwa ungependa kuendelea kujifahamisha.

WFCP20230531